• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Simanjiro

Wilaya ya Simanjiro

Wilaya ya Simanjiro ni kati ya Wilaya tano (5) zinazounda Mkoa wa Manyara, ilianzishwa mwaka 1993 ikigawanywa kutoka Wilaya ya Kiteto. Wilaya inapakana na Wilaya ya Monduli upande wa Kaskazini Magharibi; Arumeru, Hai na Moshi upande wa Kaskazini; Kiteto upande wa Kusini; Kondoa na Babati upande wa Magharibi; na Mwanga, Same, Kilindi na Korogwe upande wa Mashariki. Wilaya ina eneo lenye ukubwa wa jumla ya kilometa za mraba 20,591. Wilaya ya Simanjiro imejaliwa kuwa na madini ya vito na ni eneo pekee duniani lenye madini ya Tanzanite.

Jiografia na hali ya hewa ya Wilaya

Wilaya iko katika eneo la nyanda kame na mbuga, hupata mvua za wastani wa kati ya milimita 400 na 500 kwa mwaka. Wilaya ina vipindi viwili vya mvua ambavyo ni vuli na masika.  Mvua za vuli hunyesha kuanzia mwezi Novemba hadi Desemba na masika hunyesha kuanzia mwezi Machi hadi Mei.

Utawala, idadi ya watu na pato la Mwananchi

Utawala

Wilaya ya Simanjiro ina Tarafa sita (6), Kata kumi na nane (18), Vijiji hamsini na sita (56) na Vitongoji mia mbili sabini na nane (278).

Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na jumla ya wakazi 178,693, kati yao Wanawake ni 89,718 na Wanaume ni 88,975. Kwa mwaka 2021 Wilaya ilikadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 222,842 kati yao wanawake 113,649 na wanaume 109,193 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 3.2 kwa mwaka.

Hali ya Uchumi

Pato la Mkazi (D-GDP) kwa mwaka 2010 lilikadiriwa kuwa shilingi 268,000 na sasa linakadiriwa kufikia Shilingi 478,375 ikiwa ni ongezeko la asilimia 56.02. Shughuli kuu zinazowapatia kipato wakazi wa Simanjiro ni pamoja na Ufugaji (80%), Kilimo, Uchimbaji wa Madini, Uvuvi, Utalii na Viwanda vidogo vidogo (20%).

Fursa za Uwekezaji katika Wilaya ya Simanjiro

Serikali katika Wilaya ya Simanjiro imejielekeza katika kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya kijamii ili kukuza mazingira wezeshi ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa wananchi kama vile uboreshaji wa vituo vya afya, zahanati na Hospitali ya Wilaya, kuanzishwa kwa miradi ya maji katika Vijiji na miradi mikubwa ya maji katika Miji midogo ya Orkesumet na  Mirerani, ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya barabara, Usambazaji wa umeme Vijijini kupitia mradi wa REA awamu ya tatu na uanzishwaji wa ujenzi wa mradi mkakati wa Mji wa kimadini (Mirerani Tanzanite City). Maboresho haya yanazidi kuyafanya mazingira ya uwekezaji kuwa rafiki zaidi kwa wajasiriamali na wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo.

Kilimo

Wilaya ina ekari 1,500,000 zifaazo kwa kilimo cha mazao ya biashara na chakula. Kati ya hizo, takribani ekari 395,000 sawa na asilimia 26.3 hutumika kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Wilaya ina miundombinu ya umwagiliaji katika vijiji 8 ambavyo ni Ngage, Lemkuna, Kambi ya Chokaa, Gunge, Shambarai, Loiborsoit B, Londoto na Kiruani.

 

Barabara

Wilaya ina mtandao wa Barabara upatao km 1971.71. Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya km 603.1 katika Wilaya ya Simanjiro, kati ya hizo km 16.7 ni za lami na km 586.4 ni za changarawe. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) anahudumia mtandao wa Barabara upatao km 1368.61. Barabara zinazohudumiwa na TARURA umegawanyika katika makundi 2 ambayo ni Barabara Ujazio (Feeder Roads) km 632.57 na Barabara za jamii (Community Roads) km 736.04.

Elimu.

Wilaya ina shule za msingi 99, kati ya hizo za serikali ni 84 na zisizo za serikali ni 15. Wilaya ina Shule za sekondari 19, kati ya hizo za serikali ni 16 na zisizo za serikali ni 3.

Afya

Wilaya ina Hospitali mbili, moja inayomilikiwa na serikali na moja inamilikiwa na kanisa la KKKT. Vituo vya afya vipo 4, kati ya hivyo 3 vinamilikiwa na serikali na 1 kinamilikiwa na shirika la dini. Wilaya ina jumla ya Zahanati 45, kati yake 38 zinamilikiwa na serikali, 5 zinamilikiwa na mashirika ya dini, 1 inamilikiwa na watu binafsi na 1 inamilikiwa na Taasisi ya Umma (TANESCO).

MADINI

Sekta ya madini ya Tanzanite ni miongoni wa sekta muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Simanjiro pamoja na uchangiaji pato la Taifa ambapo kutokana na umuhimu wake Serikali ilijenga ukuta wenye urefu wa km 24.5 ili kuyalinda ipasavyo madini haya adhimu, kipekee na dawamu duniani.  Kuanzia tarehe 15.10.2021 vibali vya kusafirisha Madini ya Tanzanite nje ya Nchi (export permit) vilianza kutolewa Ofisi ya Madini Mirerani.  

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.