• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

WATUMISHI MBULU WAWEKWA RUMANDE

Imechapishwa Tarehe: October 10th, 2018

 Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.William Ole-Nasha ametoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh.Chelestine Mofuga kuwachukulia hatua watumishi watano wa serikali akiwemo  msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi ambaye ni fundi sanifu  Moses Nguvava, Mkuu wa shule ya sekondari Tumati Bw.Killian John, Afisa Elimu sekondari Bw.Ludovick longino ,Afisa ugavi wa Wilaya Bw Faustine Safari na Mwenyekiti wa bodi ya shule ambaye ni mwakilishi wa wananchi Byrson Panga.

 akitoa taarifa ya ujenzi kwa  fundi sanifu ambaye ni msimazi mkuu wa mradi huo alisema fedha zilizoletwa na Wizara zilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3, bweni 1 na matundu ya vyoo sita ila wao kwasababu walikuta baadhi ya majengo yamekwisha jengwa na wananchi hivyo waliamua kufanya ukarabati na kukamilisha bweni moja na kuweka samani, madarasa manne  ambayo yamegharimu jumla ya shilingi milioni 29 kuongeza vyoo na mabafu kwenye mabweni   million 18 na kukamilisha maktaba ambayo imegharimu million 15.

Awali kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Mofuga alisema “Serikali imetoa hizi hela kwa kusaidia na kuongeza nguvu kwa wananchi nimesikitishwa na matumizi haya hivyo nakuagiza OCD kuwakamata wahusika wote wa ujenzi ndani ya masaa arobaini na nane na baada ya hapo wafunguliwe mashtaka kwa mujibu wa sheria na pia nawaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina namtaka Mkurugenzi aniletee taarifa ya kina juu ya mradi huu”alisistiza

 Aidha akizungumza na watumishi wa shule,wanafunzi,wananchi  pamoja na viongozi wa serikali alipokuwa akikagua  mradi wa ujenzi katika shule ya sekondari Tumati Mh .Naibu Waziri alisema  “ huu ni utumiaji vibaya  wa fedha za serikali kwani jumla ya million 141 zilitolewa kwa ajili ya ajili ya ujenzi wa madarasa 3 mapya , bweni1, na matundu sita ya choo haziwezi kutumika kukarabati majengo ambayo tayari yamejengwa kwa nguvu za wananchi hivyo nimesikitishwa sana na matumizi haya ya fedha kwani wametumia nyingi hivyo serikali ya awamu ya tano haiwezi kuvumilia ubadhilifu wa fedha na hatua zitachukuliwa iwe funzo kwa wengine.

Akihitimisha ziara yake katika Halamashauri ya Wilaya ya Mbulu aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzitumia rasilimali zinazoletwa na Seikali kwa ajili ya manufaa yao, pia alizitaka Halmashauri zote  kuzitumia vizuri fedha wanazopewa na serikali  pamoja na kufuata maagizo ya wizara na vilevile aliwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kuwapeleka watoto shule kwani wakiwaacha nyumbani wanawanyima haki yao ya msingi ya kusoma.

(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.