• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

TAKUKURU MANYARA YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA

Imechapishwa Tarehe: November 30th, 2018

Taasisi ya kuzuaia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2018, imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 270,973,774.48 zilizokuwa zimefanyiwa ujanja ujanja kutoka kwenye miradi mbambali inayotekelezwa mkoani hapa na kuzirejesha serikalini na zingine kuzielekeza kwenye miradi husika.

Pia Taasisi hiyo imeanzisha utaratibu wa kufuatilia fedha zote zinazotolewa na serikali pamoja na wafadhili kwa ajili ya huduma na miradi ya Maendeleo kuanzia bajeti  zinapopitishwa,zinapo pokelewa au  kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani na kufuatilia mchakato wa matumizi au manunuzi unapofanyika na katika hatua zote za utekelezaji wa mradi husika.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Mkuu wa TAKUKURU Fidelis Kalungura, amesema katika ufuatiliaji huo watahakikisha wanadhibiti ucheweleweshaji katika uanzishaji wa mchakato wa matumizi mara baada ya fedha kupokelewa au kukusanywa kwani mchakato wa matumizi na manunuzi mara nyingi yamekuwa yakiathiriwa na vitendo vya rushwa.

Aidha Kalungura amesema TAKUKURU mkoani Manyara itakuwa makini katika kusimamia  hatua ya utekelezaji wa mradi ili pasitokee uvujaji au uchepuzi na fedha ili kuhakikisha mradi husika unakamilika ukiwa unalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

Amesema jumla ya miradi 71 yenye thamani ya shilingi Bilioni 47.8 inayotekelezwa mkoani Manyara inafuatiliwa ambapo inajumuisha miradi 48 ya maji,miradi 8 ya Afya,miradi 9 ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu,mradi mmoja (1) wa ofisi ya Halmashauri ya Kiteto,ujenzi wa jingo moja (1) la mazoezi VETA,ujenzi wa Ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Matufa,mradi wa mtaa wa viwanda SIDO,mradi wa mtandao wa bara bara awamu ya pili zenye urefu wa Km. 4.108 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Magara.

Mkuu huyo amesema TAKUKURU mkoani Manyara imejipanga kuzuia Rushwa kwa kufatilia fedha zote zinazotolewa na serikali,wafaadhili na zitokanazo na makusanyo ya ndani kwa ajili ya huduma na maendeleo, na kuongeza kuwa itaendelea kushirikiana na  jamii katika mapambano ya rushwa pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusiana na Rushwa.

Imeandikwa Na: John Walter

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.