• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

SAMBAZENI MBOLEA KWA WAKULIMA-MAKAMU WA RAIS

Imechapishwa Tarehe: November 17th, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amewataka wazalishaji wa mbolea kuendelea na uzalishaji wa mbolea kwa wingi na kujitahidi kusambaza mbolea hizo kwa wakulima ili kuongeza mazao mashambani

Makamu wa Rais ameyasema hayo akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake  alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mbolea huko Mnjingu Mkoani Manyara.

Kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bwana Toxic Hans alisema kuwa kiwanda cha Minjingu kimesaidia jamii ya Kijiji cha Minjingu kwa kujenga zahanati,madarasa, na kusaidia mradi wa maji kwa wananchi wa kijiji hicho.

Vilevile Makamu wa Rais aliwataka wazalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho kuacha mara moja kuweka mbolea katika mifuko yenye nembo ya nje ya nchi kwa mbolea hiyo inazalishwa Tanzania. “Nawapongeza kwa juhudi zenu mnazozifanya kuzalisha mbolea kwa wakulima wetu lakini achani tabia ya kuweka mbolea kwenye mifuko yenye nembo ya nje ya Nchi” Mama Samia alisisitiza.

Mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Makamu wa Rais alitembelea Ofisi za Mamlaka ya Maji Safi mjini Babati (BAWASSA) na kulizindua rasmi.

Mheshimiwa Makamu  wa Rais aliwapongeza Viongozi kwa ujenzi wa jengo la kisasa na kuwataka BAWASSA kuhakikisha Mamlaka inaongeza mtandao wa maji ili kuwa na wateja wengi na kujiongezea mapato.

Mama Samia pia alitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara na kuweka jiwe la msingi na kupongeza ujenzi wa Hospitali hiyo unavyotumia gharama ndogo kama fedha zitasimamiwa vizuri.

Baada ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara alitembelea na kuzindua Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Babati na kufanya mkutano wa hadhara kwa kuongea na wananchi katika uwanja wa Kwaraa.

Ziara ya Makamu wa Rais itaendelea tena tarehe 18/11/2018 kwa kutembelea Wilaya ya Hanang.

(Kwa picha mbalimbali na Video angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)

Imeandikwa Na: Haji A. Msovu

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.