• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mnyeti aaga rasmi Manyara, Mkirikiti Aingia

Imechapishwa Tarehe: July 23rd, 2020

            Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiwa katika hafla ya kumkaribisha rasmi katika Ofisi ya Mkuu ya Mkuu wa Mkoa Julai 23,2020.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alezander Pastory Mnyeti leo Alhamis Julai 23, 2020 ameaga rasmi kwa watumishi na wananchi wote wa Mkoa wa Manyara wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa mpya Mh. Joseph Joseph Mkirikiti aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli.

Akionekana mwenye furaha Mh.Mnyeti aliwaambia wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi kuwa  Mkoa wa Manyara kwa upo katika hali nzuri ya usala na hakuna matukio ya kutishia wananchi na mali zao na kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii wakifuata sharia zilizowekwa na serikali ili kujiongezea kipato cha kila siku.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Joseph Mkirikiti (kushoto) alipokuwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Alexander P.Mnyeti wakati wa hafla makabidhiano ya Ofisi Julai 23,2020.

Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za serikali Mh.Mnyeti alisema katika kipindi chake cha kuwepo Manyara kama Mkuu wa Mkoa  taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2018/2019 zilionesha kuendelea kuimarika kwa usimamizi wa fedha za Serikali katika sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sekretarieti na Halmashauri zote saba za Mkoa wa Manyara zilipata hati safi, hivyo kumuumba Mkuu wa Mkoa mpya ahakikishe anazisimamia Halmashauri ili ziendelee kuwa na hati safi.

 “Naomba nitumie nafasi hii kukupongeza kwa kuaminiwa na Mh.Rais Dkt.John Pombe Magufuli hadi kufikia hatua ya kuteuliwa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa kutoka nafasi ya Mkuu wa wilaya uliyokuwa nayo hapo awali.Heshima uliyopewa kubwa na ni imani yangu kuwa utaimudu kikamilifu kwani najua utendaji wako wa kazi. Nimwfanya kazi na wewe kwa ukaribu kwa takribani miaka mitatu, mimi nikiwa Mkuu wa Mkoa na wewe ukiwa Mkuu wa wilaya ya Hanang.Pamoja na pongezi hizi,tambua kuwa kuna kazia ambazo sikuweza kuzimaliza na zinahitaji msukumo wako ili ziweze kukamilika’’ Alisema Mh.Mnyeti.

Baadhi ya watumishi na viongozi wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Pamoja na kumkabidhi Ofisi Mkuu wa Mkoa mpya Mh.Mnyeti pia aliwashukuru wakuu wote wa Sehemu na Vitengo,Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,Wakuu wa wilaya zote tano za Mkoa,Wakurugenzi wa Halmashauri zote wafanyakazi wote katika Mkoa wa Manyara kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa Manyara.

Baadhi ya watumishi na viongozi wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Kamati ya siasa Mkoa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

“Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwasamehe wote walionikosea na mimi kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea kwani yalikuwa ni sehemu ya majukumu ya kazi na Mwenyezi Mungu akijalia tutaendelea kuwasiliana” Alimalizia Mh.Mnyeti.

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali zilizopo Mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joseph Joseph Mkirikiti alimpongeza sana Mkuu wa Mkoa anayeondoka kwa kazi kubwa aliyoifanya Mkoani Manyara katika mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama,kutatua migogoro ya ardhi katika Mkoa na kuhimiza shughuli za maendeleo.

 “Mheshimiwa Mnyeti naomba nikuhakikishie kuwa ulipoishia ndipo nitakapoanzai kwa kushirikiana na timu nzima uliyoniachia.Lakini ifahamike kuwa nidhamu,heshima, maadili mema na uwajibikaji pamoja na kumtegemea Mungu ndiyo mambo pekee yatakayotufikisha kwenye mafanikio na kuepukana na migogoro isiyo ya lazima” Alisema Mh.Mkirikiti.

Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joseph Joseph Mkirikiti na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mh.Alexander Mnyeti.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara Simon Lulu (kulia) akimkabidhi zawadi aliyekuwa Mkuu wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti.

Wakitoa salama mbalimbali Mwakilishi wa Wafanyakazi kutoka Sekretarieti ya Mkoa,Mkuu  wa Wilaya ya Simanjiro, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara,Mkurugenzi wa Mji wa Babati,Paroko wa Kanisa Katoliki na Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi Mkoa Mh.Simon Lulu walimshukuru sana Mh.Mnyeti kwa ushirikiano wake na kumtakia kila la heri huko aendako.

Mheshimiwa Mnyeti amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara tangu tarehe 26 Oktoba 2017 hadi tarehe 25 Julai 2020 alipoteuliwa Mheshimiwa Joseph Joseph Mkirikiti kuchukua nafafi yake.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Manyara Mh.Alexander Mnyeti (kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Musa Missaile.

Mkuu wa Mkoa Manyara Mh.Joseph Joseph Mkirikiti (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara Bwana Simon Lulu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Manyara Mh.Alexander Mnyeti (katikati) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bwana Fortunatus Fwema (kushoto)  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Musa Missaile.

(Kwa Picha mbalimbali za hafla ya makabidhiano kati ya Mh.Mnyeti na Mh.Mkirikiti angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Imeandikwa Na:Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.