• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

MANYARA KUWA NA MIKOA MIWILI YA KIMADINI

Imechapishwa Tarehe: November 15th, 2018

Mkoa wa Manyara umegawanywa katika mikoa miwili ya ya kimadini ambayo ni Manyara na Simanjiro kutokana na upatikanaji mkubwa wa aina mbalimbali za madini yanayopatina kwa wingi Mkoani Manyara.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa madini Mh. Anjela Kairuki alipokuwa Wilayani Simanjiro katika ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan.

Waziri Kairuki alisema kwa kuwa Mkoa wa Manyara umebarikiwa aina mbalimbali za madini Wizara ya madini imeamua kutenga Mkoa mpya wa Kimadini ambao makao Makuu yake yatakuwa Mirerani ili kuongeza ufanisi wa kazi za madini katika Mkoa huo.

Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake  Mkoani Manyara Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan alitembelea na kukagua ukuta katika enero la Madini ya Tanzanite lililopo Mirerani na pia alitembelea kiwanda cha madini ya Kinywe (Graphite) pia kilichopo hukohuko Mirerani Wilayani Simanjiro na kuweka jiwela msingi la kiwanda hicho.

Akiongea na wamiliki pamoja na  wafanyakazi wa kiwanda hicho Mhe.Makamu wa Rais aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa madini ya Kinywe kwani hicho ndo kiwanda pekee kinachozalisha madini ya Kinywe nchini Tanzania.

Madini ya Kinywe yanatumika kutengezea betri za magari,betri za simu pamoja na betri za saa,Vipuli vya mitambo pamoja na kutunza umeme kwa muda mrefu.

Akiongea kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Mkuu wa Mkoa wa Manyara alisema kuwa Mkoa wa Manyara upo katika hatua za mwisho za kukamilisha idadi ya viwanda mia kwa kila mkoa katika kutimiza kauli mbiu ya “Mkoa wangu Kiwanda changu”

Mara baada ya kutembelea kiwanda cha Graphite Makamu wa Rais alifanya mkutano wa hadhara katika Mji wa Orkesumet kwa kuongea na wananchi wa wilaya ya Simanjiro.

Katika mkutano huo aliwataka wananchi kupambana na udumavu,maradhi ya ukimwi,ukeketaji na kuacha kuwaozesha watoto katika umri mdogo.

Kwa upande wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa  Mh.Suleiman Jafo alisema kuwa Serikali tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Simanjiro pamoja na Jengo la Halmashauri ya Wilaya kabla ya Juni 2019.

Ziara ya Makamu wa Rais inaendelea tarehe 16 Novemba wilayani Babati.

(Kwa picha mbalimbali na Video angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)

Imeandikwa Na: Haji A. Msovu

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.