• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YANATISHIA JAMII

Imechapishwa Tarehe: November 28th, 2018

Watu milioni 7.6 kila mwaka duniani hupoteza maisha kutokana na  magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu huku milioni  92 wakiathiriwa na Magonjwa hayo.

Hayo yamesemwa na Daktari wa Upasuaji kutoka hospitali ya rufaa ya  mkoa wa Manyara Dr.Ezekiel Morris Lukenza wakati akitoa mafunzo kwa Magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza kwa watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu kanda ya Kati (TFS) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Dr. Lukenza amesema magonjwa hayo yanashambulia jamii na kuongeza gharama ya maisha  ambapo ugonjwa wa Shinikizo la damu ndio unaongoza kupoteza nguvu kazi ya  taifa.

Aidha Dr.Lukeza amesema ili jamii iweze kuepuka maradhi ya Moyo, kisukari na Ukimwi lazima  kupima afya  mara kwa mara kuuweka mwili vizuri kwa kufanya mazoezi na kuzingatia matumizi ya dawa pindi unapogundulika.

Pia amewataka watanzania kubadilisha mitindo ya maisha wanayoishi kwani ndio chanzo kikubwa cha kupata magonjwa haya yanayopoteza maisha ya wengi.

Naye Meneja Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu kanda ya kati Dodoma (TFS) Haji  Khatibu, amesema katika  mipango na bajeti  wameweka shughuli za Mafunzo yanayohusu Magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza kama vile ukimwi na Shinikizo la Damu  kwa watumishi wake ili wafahamu namna ya kujilinda  na kuchukua hatua ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Amesema ni mpango wao wa kila mwaka kutoa Mafunzo ya aina hiyo  kwa watumishi wa wakala wa Misitu ili kuimarisha utendaji wa kazi na kuwakumbusha kuwa Magonjwa hayo ni  hatari kwa afya zao ambapo wanawatumia wataalamu wa afya katika mafunzo hayo.

Sambamba na hayo Wataalamu hao wa Misitu kutoka kanda ya kati inayohusisha mikoa ya Manyara,Arusha,Dodoma na Singida walipima na kuchangia benki ya damu.

Amesema wengine wanaweza kuona wanatumia rasilimali fedha lakini wao wanaamini Kinga ni bora kuliko Tiba hivyo wataendelea na utaratibu huo.

Aidha Haji amewataka watumishi hao wazingatie yote waliyofundishwa kwa kuyatilia mkazo kwa vitendo zaidi.

Akiyafunga mafunzo hayo ya siku mbili yaliyolenga kutoa elimu ya Rushwa na Afya,Katibu tawala wa mkoa wa Manyara Missaile Raymond  Musa amewataka watumie fursa hiyo kama chachu ya kuepuka vitendo vya rushwa  vinavyosababisha mazao ya misitu kupitishwa kimagendo.

Amesema mazao ya misitu kama zilivyo rasilimali nyingine za taifa ni muhimu katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja pamoja na kuongeza ajira.

Ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Wakala wa huduma za  Misitu kanda ya kati kwa kuuchagua mkoa wa Manyara kwa mara ya pili mfululizo kufanyia mafunzo ya magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza na kwa sababu imechangia kwenye pato la mkoa kwa huduma mbalimbali walizozipata na kuongeza mahusiano mazuri ya kitaasisi.


Imeandikwa Na: John Walter

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Miaka Miwili ya Rais Samia Manyara ni Shangwe tupu Miradi ya Maendeleo

    March 18, 2023
  • SERIKALI YATOA MAAGIZO MGOGORO WA ARDHI KIRU

    February 13, 2023
  • MITI MILIONI 10.5 KUPANDWA MANYARA

    January 27, 2023
  • RC MAKONGORO AMESEMA WALIOCHAGULIWA WATAINGIA DARASANI BILA USUMBUFU WOWOTE

    January 23, 2023
  • Tazama Zote

Video

Karibu Mwenge wa Uhuru 2022 Mkoa wa Manyara
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.