Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexanda Mnyeti alifanya mkutano na wananchi wa kitongoji cha Katikati katika kata ya Komoro Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakumba wananchi wa kitongoji hicho ikiwemo kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka kumi ambapo vijiji vya Gitiangari na Sukro vilikuwa vikigombania kitogoji cha Katikati.
Awali akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Katikati aliwashukuru kwa uvumilivu,busara na hekima walizozitumia katika kupigania haki ya kitongoji chao,Mh.Mnyeti alisema” ni zaidi ya miaka kumi sasa mgogoro huu wa ardhi umekuwa ni kero hii ni kutokana na siasa zisoleta maendeleo hivyo kuwafanya wananchi kushindwa kuendelea kujikwamua kiuchumi na haya ni majibu kutoka serikali kuu kitongoji cha Katikati kibaki katika kijiji cha Sukuro" Alisisitiza.
Aidha wakitoa maoni mbalimbali Abraham Koringo na Lengai Lazaro waliishukuru serikali kwa maamuzi waliyoyatoa kwani ni muda wa miaka kumi wamekuwa wakihangaika kutatua mgogoro huo lakini wamekuwa wakiyumbishwa na wanasiasa hivyo kukwamisha juhudi mbali mbali za kimaendeleo zilizokuwa zinafanywa na wananchi.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Barabara ya Babati - Singida
Anuani ya Posta: P.O.BOX 310
Simu ya mezani: 027-2510066
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: rasmanyara.go.tz
Copyright ©2020 Manyara Region . All rights reserved.