• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Misri kuwekeza kwenye kilimo nchini

Imechapishwa Tarehe: February 6th, 2019

Ujumbe kutoka serikali ya Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo na ardhi wa nchi hiyo Dkt Ezzidine Abu Stiet upo nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ziara ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Ukiwa nchini ujumbe huo mbali na kuonana na viongozi wa Wizara ya kilimo, ulipata fursa ya kuonana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege ambapo ulimweleza Naibu Waziri juu ya azma yao ya kutaka kuwekeza katika sekta za kilimo, na ufugaji wa kuku.

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa kilimo na ardhi, Serikali ya Misri ingependa kuwekeza mojawapo kati ya mazao makuu matatu ambayo ni ngano, mpunga au miwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mhe.Kandege aliupongeza ujumbe huo kwa nia yao ya kuwekeza katika kilimo nchini.

Waziri huyo wa kilimo wa Misri alifuatana na Mkuu wa kituo  cha utafiti wa kilimo cha Misri Dkt Mohamed Soliman Mohamed,  Meneja Mtendaji wa mashamba ya ushirikiano katika nchi za kiafrika Dkt Maher El Maghraby na Mkuu wa sehemu ya utafiti wa ngano kutoka taasisi ya utafiti wa mazao Dkt Salah Abd El-Megied Makady.

Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe.Abdulwafa, Afisa Ubalozi wa Misri Bwana Ahmed, Meneja wa shamba la ushirikiano Zanzibar Dkt Reda Abdallah Abdelaziz, na Afisa wa shamba la ushirikiano la zanzibar anayehusika na uhandisi wa kilimo Dkt Yoursry Abdelkawy Sahan.

Wengine ni bwana Abbas Ngwale kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Misri na Bi Elizabeth Rwitunga afisa dawati wa Misri, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Na Mathew Kwembe, Majid Abdukarim,

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Vijana Kiteto wanufaika na Mikopo ya Halmashauri

    January 05, 2021
  • Babati watakiwa kuchangamkia Mikopo ya Serikali

    January 04, 2021
  • Waziri wa Kilimo awataka Wakulima wa ngano kuongeza uzalishaji

    December 24, 2020
  • Njooni muwekeze Manyara- RC Manyara

    December 22, 2020
  • Tazama Zote

Video

Nangwa Sekondari katika muonekano mpya
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2020 Manyara Region . All rights reserved.