Makamu Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (R) Mbarouk Salum Mbarouk amefungua mkutano wa wadau Mkoani Manyara leo ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
Wadau wa Tume Mkoani Manyara wanaoshiriki mkutano huo wanatoka katika makundi mbalimbali yakiwemo ya vyama vya siasa,viongozi wa dini wawakilishi wa watu wenye ulemavu,wanawake,vijana,wajasiriamali na asasi mbalimbali za kiraia.
Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura katika Mkoa wa Manyara utaanza rasmi katika Halmashauri zote saba kuanzia Tarehe 31/07/2019.
Zoezi hilo litawahusu :-
1.Raia wenye miaka 18 au watakaofikisha umri wa miaka 18 ifikakapo muda wa uchaguzi (Oktoba 2020).
2.Wapiga kura walihamia kutoka sehemu moja kwenda nyingine
3.Kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa.
4.Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao au kadi zao kuharibika.
#TUKUTANE VITUONI!!!
Barabara ya Babati - Singida
Anuani ya Posta: P.O.BOX 310
Simu ya mezani: 027-2510066
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: rasmanyara.go.tz
Copyright ©2021 Manyara Region . All rights reserved.