• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakika Kiteto Mkuu wa Mkoa aitaka Tanesco kumaliza kero ya Umeme

Imechapishwa Tarehe: February 8th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti amemuagiza Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kiteto Mhandisi Lazaro Lenoy kuhakikisha anatatua kero za upatikanaji wa umeme katika wilaya hiyo ili wananchi waweze kujipatia huduma muhimu ikiwemo upatikanaji wa maji.

Mhe.Mkirikiti ameyasema hayo jana alipokuwa akikagua miradi ya maji inayosimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kiteto.

“Tatizo la umeme katika wilaya ya Kiteto limesababisha wananchi wetu kukosa huduma muhimu ikiwe maji, kwa hiyo nawaagiza Tanesco Kiteto kumaliza hizi kero za upatikanaji wa umeme ili RUWASA ipeleke maji kwa wananchi hawa kwa urahisi” Alisema Mhe.Mkirikiti

Akielezea jinsi RUWASA inavyotekeleza miradi ya maji wilayani humo Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Kiteto Mhandisi Stephano Mbaruku amesema kuwa RUWASA mwaka 2021 inakusudia kuwapelekea maji wakazi 275,916 ukilinganisha na wakazi 92,080 ya mwaka 2019 na hadi kufikia mwaka 2023 inatarajiwa kuwafikia wakazi wa vijiji 28 vilivyobaki.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa RUWASA Wilaya ya Kiteto imepokea shilingi 169,346,810 kwa ajili ya kumalizia utekelezaji wa kazi za ujenzi wa miradi ya maji ya wezamtima na Ostet na miradi hii ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ili huduma ya maji ipatikane kama ilivyokusudiwa” Alisema Mhandisi Mbaraku.

Pamoja na Miradi ya maji ya Wezamtima na Ostet RUWASA wilayani Kiteto pia imetekeleza miradi ya maji ya Matui wenye gharama 692,918,911, mradi wa Mdinku wenye gharama ya shilingi 168,108,923.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi wa Kiteto lakini kuna changamoto ya kutokuwepo au kukatika mara kwa mara kwa nishati ya umeme hali inayopelekea mashine za Kusuma maji kushindwa kufanya kazi” Aliongeza Mhandi huyo wa RUWASA Wilaya ya Kiteto.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Manyara ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Bwana Jacob Siay ameonesha kuridhishwa na jinsi RUWASA inavyotekeleza Ilani ya Chama kwa kuhakikisha wananchi katika Vijiji vyote wanapata huduma ya  maji safi na salama na kuwashauri wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha wanatunza miundombinu ya maji.

“Kiukweli sisi kama kama kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara tumeridhishwa na jinsi RUWASA inavyotekeleza miradi ya maji na sisi tunataka kuona ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa katika sekta mbalimbali” Alisisitiza Bwana Jacob Siay.

Katika Wilaya ya Kiteto Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Joseph Mkirikiti akiambatana na Kamati ya Siasa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa huo bwana Musa Missaile wamekagua miradi minne kati ya miradi nane inayotekelezwa na RUWASA kwa mwaka 2021.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Mkuu wa Mkoa afurahishwa na Mradi wa Maji wa Bilioni mbili

    February 09, 2021
  • Ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakika Kiteto Mkuu wa Mkoa aitaka Tanesco kumaliza kero ya Umeme

    February 08, 2021
  • RUWASA Kumaliza shida ya Maji Manyara

    February 06, 2021
  • Waziri Mkuu ashiriki mazishi ya Mbunge Manyara

    January 26, 2021
  • Tazama Zote

Video

Asilimia mbili ya mikopo kwa walemavu
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2021 Manyara Region . All rights reserved.