Mkoa wa Manyara ulianzishwa mwezi July mwaka 2002, na Makao Makuu ya Mkoa yako kwenye Mji wa Babati, umbali wa Km.167 kutoka mji wa Arusha kupitia barabara kuu ya Kaskazini itokayo Arusha kwenda Dodoma na Singida. Mji wa Babati uko katika njia panda ya kwenda Singida na Dodoma umbali wa Km.163 kutoka Singida na Km.164 kutoka Dodoma.
HARAMBEE YA ELIMU MKOANI MANYARA Mkoa wa Manyara ni moja kati ya mikoa iliyo nyuma kielimu. Ili kukabiliana na tatizo hili Mkoa umejiwekea mkakatiendelevu wa kusimamia na kushauri Halmashauri kuweza
kuboresha mazingira ya kutolea na kuendeleza elimu kwa ujumla. Mkakati huu ni pamoja na kuanzisha Mfuko wa Elimu wa Mkoa utakaosaidia kwa haraka kuboresha miundombinu ya elimu ambayo ni mabweni, dahalia, maabara, vyumba vya madarasa na nyumba za walimu ambavyo ni michache.
Katika kutekeleza mkakati huu Mkoa na Wilaya imejiwekea malengo ya kuchangia nguvu na fedha ili kuharakisha uboreshaji huo.